ad

ad

Nandy Ajivunia Kolabo na Aslay

Faustina Charles ‘Nandy’ .
 STAA wa muziki wa Bongo Fleva, Faustina Charles ‘Nandy’ ameeleza kuwa anajivunia kufanya kolabo na msanii mwenzake ambaye yupo juu kwa sasa kwenye gemu, Dogo Aslay kwa kuwa anamkubali siku nyingi Akichezesha taya na Mikito Nusunusu, Nandy ambaye ameshirikishwa kwenye wimbo wa Aslay aliouachia mwanzoni mwa wiki hii unaokwenda kwa jina la Mahabuba alisema ni jambo la kujivunia kwake kufanya kazi na msanii huyo kwa kuwa anafanya vizuri kwa sasa na anakubalika kila kona.   “Nimefurahi sana kufanya kazi na Aslay, najivunia sana sababu wasanii wa kike wapo wengi lakini katika kipindi kama hiki ambacho Aslay anakimbiza kwenye gemu akaona afanye ngoma na mimi, nawasihi mashabiki wangu watarajie makubwa zaidi ya hayo,” alisema. 
STORI NA MAYASA MARIWATA - GPL

No comments

Powered by Blogger.