ad

ad

Singida United Yafanya Kweli Nyumbani, Yaitandika Timu Ya Matola

Ligi Kuu ya Vodacom imeendelea leo Ijumaa kwa kuchezwa mchezo mmoja mkoani Singida.

Timu ya Singida United ikiwa nyumbani, imefanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Lipuli United katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom uliocheza kwenye Uwanja wa Namfua.
Hadi dakika 45 zinakamilika timu hizo zilikuwa nguvu sawa kwa matokeo ya 0-0 huku zikishambuliana kwa zamu.

Kipindi cha pili wenyeji walicheza vizuri na kufanikiwa kupata bao la ushindi katika dakika ya 82 kupitia kwa Danny Usengimana.

Kwa ushindi huo sasa Singida inayofundishwa na Hans van Pluim imefikisha pointi 17 katika michezo 10, Lipuli inayonolewa na kiungo wa zamani wa Simba na Taifa Stars, Selemani Matola imeendelea kubaki na pointi 13 katika michezo 10. 

No comments

Powered by Blogger.