ad

ad

Mke wa Mwanajeshi: Sasha Kanipora Mume Wangu, Mke Asimulia Mazito

 
Mama aliyejitambulisha kwa jina la Rehema Zuberi ‘Mama Asia’.

NI skendo nzito ya kufungulia mwaka 2018! Mama aliyejitambulisha kwa jina la Rehema Zuberi ‘Mama Asia’ ambaye ni mke wa mwanajeshi mstaafu aliyemtaja kwa jina la Abdulrahman amelia na kutoa madai mazito ya kuporwa mumewe huyo na Video Queen wa Kibongo, Sasha Kassim. Mama huyo alitamka: “Jamani nisaidie Shasha kanipora mume wangu na naona amehamia kabisa nyumbani kwangu baada ya mimi kuondoka.”
Video Queen wa Kibongo, Sasha Kassim.
MAPICHAPICHA TEGETA
Akiangua kilio mbele ya Risasi Jumamosi, Mama Asia alisema kuwa, kinachomuuma na kumkera zaidi ni kitendo cha Sasha kupiga picha akiwa kwenye nyumba yao iliyopo Tegeta jijini Dar na kujitapa kuwa yupo kwake ilihali akijua kuwa yupo kwa mume wa mtu. “Yaani nyumba yangu ilikuwa ‘ikiwaka moto’ kindoa hivyo ikafika wakati mume wangu akanitaka niondoke na watoto.
[caption id="attachment_193455" align="aligncenter" width="351"]  
Mwanajeshi mstaafu aliyemtaja kwa jina la Abdulrahman.
“Awali sikujua kama ni yeye (Sasha) kwa sababu mimi na mume wangu tulikuwa na tofauti zetu, lakini baada ya kuona Sasha kahamia na kuanza kupiga picha nyumbani hapo huku akiwa na ‘hausi boi’ wetu ndipo nilipoamini kuwa yeye ndiye aliyesababisha matatizo ndani ya ndoa yangu,” alidai mama Asia.
Siku ya ndoa yao.SASHA CHUMBANI Mama huyo aliendelea kudai kuwa, Sasha amekuwa akipiga picha za mapozi tata na kuzitupia mitandaoni akionesha mazingira ya nyumbani kwake, jambo ambalo hakulitarajia. “Bado mume wangu hajanipa talaka. Kitendo cha Sasha kuingia na kujiachia nyumbani kwangu kinaniumiza, si ujua kwako ni kwako tu, unajua kila sehemu kiasi kwamba mtu akipiga picha utajua yuko kwako, naumia sana,” alisimulia Mama Asia kwa machungu.

WAMSHANGAA SASHA
Mama Asia aliongeza kudai kuwa, wanaye wanamshangaa mno Sasha kwa kuwa na ukaribu na baba yao na akamtahadharisha kwa kumwambia kuwa, asiweke picha hizo mtandaoni kwani zinasababisha shida kwa watoto wake na kudai kwamba endapo atafikia hatua ya kumsaka, atamtafuta, lakini kwa sasa anamtumia ujumbe huo tu.
Sasha Akifanya yake.TAHADHARI KABLA YA HATARI
“Mimi sihangaiki kumsaka, kwa sasa ninamweleza tu atambue analolifanya si zuri, lakini ikifikia hatua ya kumsaka, nitamsaka,” alisema mama huyo.

MKE APEWA HIFADHI KWA KIPINGU
Mama Asia alisema kuwa, kutokana na kuwa na tofauti na mumewe, mke wa Kanali Kipingu ambaye ni rafiki yake mkubwa alimpa hifadhya nyumba ya kuishi. “Nilipopata matatizo, mke wa Kipingu alinipa sehemu ya kuishi, alinipa kibanda nyuma ya nyumba yake ndipo ninapoishi na watoto wangu kwa sasa,” alisema Mama Asia akisisitiza kuwa anapitia kwenye matatizo, lakini chanzo cha yote hayo ni Sasha.
 
Enzi za Furaha kabla ya kuchukuliwa mume wake
MZEE ABDUL SASA

Baada ya habari hizo kutua kwenye Dawati la Risasi Jumamosi, mwandishi wetu alimtafuta Mzee Abdul na kumsimulia malalamiko yote ya mkewe ambapo alifunguka ya kwake. Risasi Jumamosi: Kuna madai yametufikia hapa kuwa wewe unatoka na msichana anayeitwa Sasha ambaye amekuwa akionekana nyumbani kwako na mkeo na watoto hawapo hivyo yeye amechukua nafasi hiyo.

Je, unalizungumziaje hilo? Mzee Abdul: Ehee! Kwanza kama ni mke wangu ameleta habari hizo, hakutakiwa kufanya hivyo, alitakiwa kuja kumkamata (Sasha) hapa nyumbani ili apate ushahidi mzuri kwa sababu hajafukuzwa au angeenda mahakamani.

Risasi Jumamosi: Mama Asia anasema mna mgogoro ambao umewatenganisha, lakini anamtaja huyo Sasha kuhusika kwa sababu amemuona akipiga picha hapo nyumbani na kuziachia mitandaoni akidai yupo kwake baada ya yeye kuondoka.

Mzee Abdul: Kuhusiana na mgogoro, yeye asubiri mahakama, ameondoka mwaka na kitu, hawezi kunipangia nani aje nyumbani na nani asije na huyo Sasha simjui na wala sijawahi kumuona na ukija kwa wapangaji wangu wala hutamkuta mtu anayeitwa Sasha kwa sababu nina wapangaji wengi hapa.

Risasi Jumamosi: Lakini mama Asia anasema huyo si mpangaji, anadai ni mtu wako, hujanielewa? Mzee Abdul: Mimi ninaomba athibitishe hilo. Je, amewahi kutufuma popote? Mbona yeye amekuwa akipiga picha na watu mbalimbali? Je, hao nao ni wapenzi wake? Hata hivyo, ameona picha nipo na huyo Sasha?

Risasi Jumamosi: Picha ukiwa na Sasha hakuna, ila Sasha anaonekana amepiga akiwa ndani kwako na nyumba yako inaonekana. Mzee

Abdul: Kwani yeye (mama Asia) hana wapenzi? Hata mimi ninaweza kumsema… Aache mambo ya ajabu, anataka kunichafua
mimi. Tumetengana mwaka sasa, je, hana wanaume? Mbona mimi simfuatilii? Mwaka mzima anataka tufuatiliane? Mimi ni mtu mzima sana. Hata ukiniona huwezi kuniambia mambo ya kuwa na uhusiano na Sasha. Ninasisitiza simjui!


SASHA AJITETEA Baada ya mahojiano na Mzee Abdul kwa njia ya simu, mwandishi wetu alimtafuta Sasha ambaye alijitetea kuwa, huwa anakwenda kwenye nyumba hiyo na huenda hilo ndilo limemponza, lakini hatembei na mwanaume huyo.

Alisema kuwa, huwa anakwenda kwenye nyumba hiyo na aliwahi kukaa kwa wiki mbili kwani kuna rafiki yake aitwaye Fatma ambaye amepanga kwenye nyumba za mwanaume huyo. “Jamani mimi kilichoniponza ni kupiga picha nikiwa kwenye eneo hilo la nyumba hiyo. “Pale amepanga rafiki yangu, nimekuwa nikienda kwa ajili ya rafiki yangu ambaye aliniomba nikakae kwake kwa wiki mbili tu,” alisema Sasha.

SASHA ABANWA
Baada ya utetezi wake huo, Sasha alibanwa juu ya kusababisha kufukuzwa kwa hausi boi wa nyumba hiyo ambaye video yao ilionekana mtandaoni wakiwa wamepiga picha tata ambapo Sasha alijitetea kuwa, hausi boi huyo aliomba wapige picha na kwa kuwa hakuwa na hiyana, alimkubalia. “Nilimkubalia kijana huyo kupiga naye picha kwa sababu aliniomba na tulipiga picha za nje ya nyumba hiyo tu. Mimi ninamuomba huyo mama awe na amani. Mimi sina uhusiano na mumewe,” alisema Sasha.
STORI: Imelda Mtema na Hamida Hassan, Risasi Jumamosi

No comments

Powered by Blogger.